Taarifa kutoka vikosi vya usalama nchini Ufaransa zinasema kuwa washukiwa wanane wametiwa mbaroni, kuhusiana na mashambulio ya wiki iliyopita ambako watu kumi na saba waliuawa.
Afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo amesema kuwa washukiwa hao wanaendelea kuhojiwa kuhusiana na madai ya kuwasaidia washambuliaji wa shambulio la Paris kwa kuwabebea silaha au kuwapa usafiri.
Nchini Ujerumani, polisi wamewakamata washukiwa kadhaa wa ugaidi baada ya kufanya msako kali mjini Berlin.
Mmoja wa waliokamatwa anashukiwa kuwa kiongozi wa kundi moja la kiislamu lenye itikadi kali ambalo lilikuwa likijiandaa kufanya mashambulizo nchini Syria. Anadaiwa kuandaa mikutano ya kuchangisha pesa ili kuwasaidia magaidi wa Daesh wanaofanya jinai zao nchini Syria na Iraq.
Duru zinasema kwamba misako yote ilifanyika katika mtaa mmoja wa Kusini mwa Paris ambako mmoja wa washambuliaji alikulia.
Nchini Ujerumani, polisi wamewakamata washukiwa wa kundi la kigaidi baada ya kufanya misako mingine ndani na katika maeneo yanayozingira mji wa Berlin.
Hata hivyo polisi walisema hawakupata ushahidi kwamba walikuwa wanajiandaa kufanya mashambulizi nchini Ujerumani.
Mataifa ya Ulaya ni miongoni mwa mataifa yaliyo dhamini makundi mbalimbali ya kigaidi nchini Syria ambayo yamesabibisha vifo vya maelfu ya watu, mataifa haya yamedhamini makundi hayo ya kigaidi kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syria ambayo inasaidiwa na Jamhuri ya kiislamu ya Iran na vikosi vya majeshi vya Hizbollah. Makundi hayo ya kigaidi sasa yanaonekana kuwageuka wadhamini wao na kufanya mashambulizi katika nchi za wadhamini hao. Makundi hayo yakipokuwa yakifanya mashambulizi na mauaji nchini Syria na Iraq, vyombo vya habari vya Ulaya viliyaita makundi hayo kuwa ni wapambanaji wanaopigania Demokrasia, lakini baada ya makundi hayo kufanya mashambulizi ndani ya Ulaya, vyombo hivyo vya habari vimeanza kuyaita makundi hayo ya wapigania Demokrasia kuwa ni makundi ya kigaidi, na kwamba ni hatari kwa jamii.